We love eBooks
    Baixar VIPANDE VYA MAISHA VILIVYOPOTEA (Afrikaans Edition) pdf, epub, eBook
    Editora

    VIPANDE VYA MAISHA VILIVYOPOTEA (Afrikaans Edition)

    Por Lorna Dadi

    Sobre

    "Wakati Shantali anahangaika na kuthibitisha kama Doreen ni mtoto halisi wa Cosmas nchini India, Cosmas alikuwa tayari jijini Dar es Salaam akiendelea na shughuli zake kama kawaida. Siku moja Jumapili jioni wakiwa wanastarehe kwenye hoteli moja maarufu jijini Dar es Salaam pamoja na wamiliki wenzake wa kampuni ya Across Border Company Limited (ABC Limited), ghafla walivamiwa na polisi. Walikuwa wanajua kwamba biashara zao hazikuwa halali hivyo muda wote walikuwa wamejiandaa kwa lolote. Ujio wa wale polisi mahali pale uliwaashiria kwamba walikuwa katika hatari. Hivyo wakataka kuanza kuondoka mmoja mmoja lakini polisi waliwazuia. Katika purukushani na polisi Cosmas alifanikiwa kukimbia. Alipokuwa akikimbia nje ya hoteli hiyo alikuwa akirushiana risasi na polisi. Alipolikaribia gari lake risasi ilimpata kichwani akadondoka. Polisi wakakimbia kumchukua ili wampeleke hospitali. Kwa bahati mbaya Cosmas alifia njiani".

    "Ilikuwa Jumapili asubuhi, akiwa ameshavaa nguo zake, tulisikia kengele ya mlangoni ikiita kwa muda mrefu. Joshua`alikuwa anatoka kuelekea chini (chumba chetu kilikuwa ghorofani) na mimi nilimfuata nyuma nikiwa nimembeba mtoto. Wakati Joshua anamalizia ngazi ya mwisho, msaidizi wetu wa kazi za ndani – Kage – alijitokeza mbio kuelekea kufungua mlango wa nje. Ghafla waliingia watu wanne waliokuwa wamevalia nguo nyeusi kuanzia kichwani hadi miguuni, walivaa vitambaa vyeusi usoni ili sura zao zisijulikane. Mmoja alikimbilia juu nilipokuwa na Judy, akampokonya Judy kutoka mikononi mwangu huku akiwa ameniziba mdomo kwa kutumia kitako cha bastola ili nisitoe sauti. Judy alianza kulia kwa sauti ya juu sana. Mtu mwingine alimkamata Kage na kumziba mdomo na wawili walimmiminia risasi Joshua kifuani na kichwani akadondoka. Walitumia bastola zenye kiwambo cha kuzuia sauti hivyo hata mlinzi hakusikia. Damu zikatapakaa chini"

    “Siku moja Jumapili kama saa nne usiku nilikuwa natokea ofisini kwangu naelekea nyumbani Tabata. Kwa mbali niliwaona watoto wawili kandokando ya barabara, mmoja amelala chini, na mwingine amepakata kichwa chake analia. Nilishtuka sana. Nilipowakaribia nilisimamisha gari, nikateremka kuwafuata. Nilimkuta mtoto mmoja analia, “Mungu nisaidie, Mungu nisaidie”. Sikumuuliza jambo lolote. Nilimgusa mtoto aliyekuwa amelala chini nikagundua ana homa kali sana. Nilimbeba nikamwingiza kwenye gari langu kwenye kiti cha nyuma. Nikamwambia yule mwingine na yeye aingie kwenye gari akae na mwenzie kiti cha nyuma. Niliendesha gari kwa kasi sana kuelekea hospitali ya Mtakatifu Juanita, Kariakoo. Mtoto mgonjwa alipokelewa na aliendelea kuhudumiwa kwa haraka sana na daktari. Muda wote huu nilikuwa sijamuliza yule mwingine jambo lolote zaidi ya jina la mwenzake. Baada ya kupata majibu ya daktari ndipo nikaanza kumuliza:
    “Mtoto mzuri ulisema unaitwa nani?”
    “Bahati”
    “Usiku wote huu mlikuwa mnatokea wapi? (Huku nikimshika mkono). Haya twende kwenye gari nikupeleke nyumbani kwenu. Si unapakumbuka?”
    “Ndiyo.” Alijibu.
    Bahati alinielekeza hadi kwenye mtaa mmoja Kariakoo. Akanionesha kibaraza fulani ambapo tulimkuta mzee mmoja amekaa; alionekana kuwa ni mlinzi. Nikamuuliza ili kupata uhakika, “hapa?” Bahati aliitikia kwa kichwa.
    “Haya ngoja twende wote ili niwaeleze ndugu zako alipo Neema.” Nilimweleza yule mtoto.

    Historia za maisha yao zilitamalaki matukio yenye furaha, majonzi, chuki, mapenzi, mateso na visasi. Aghalabu matukio mengi yaliyotokea siku ya JUMAPILI yalitengeneza wasifu mpya katika historia ya maisha ya kila mmoja wao. Ni matukio hayo katika JUMAPILI za maisha yao yaliyowaachia kumbukumbu maridhawa zilizofurikwa na majeraha ya mikasa iliyowasibu. JUMAPILI ilibaki kuwa kitendawili kwao, kati yao hakuna aliyethubutu kufikiria kwamba katika maisha yake ingetokea JUMAPILI moja ambapo angeweza kuvikusanya vipande vya maisha yake vilivyokuwa vimepotea.
    Baixar eBook Link atualizado em 2017
    Talvez você seja redirecionado para outro site

    Relacionados com esse eBook

    Navegar por coleções